MSICHANA ALIYEMUUA MPENZI WAKE KATIKA AJALI YA KIZEMBE AFUNGWA JELA...

KUSHOTO: Mabaki ya gari baada ya ajali. KULIA: Eleanor Coleman.
Kijana aliyemuua rafiki yake kwenye ajali ya gari kufuatia usiku mzima wa sherehe ya sanamu amesema 'hatajisamehe mwenyewe' wakati akihukumiwa kifungo juzi.
Eleanor Coleman mwenye miaka 19, alikuwa katumia dawa za kurusha akili na bangi wakati akisherehekea na rafiki zake katikati ya mji wa Norwich huku wakiwa wamevalia nguo za vituko.
Lakini wakati akiendesha gari kuelekea nyumbani majira ya Saa 11 alfajiri gari lake aina ya Fiat Punto liliserereka kando ya barabara na kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembeni.
Gari hilo liliwaka moto na dereva wa lori Peter Jolly akafanikiwa kuokoa maisha ya Eleanor kwa kumburuta nje ya gari lake kabla ya kulipuka.
Aliomba msaada kwa wapita njia, ambao waliweza kuwatoa abiria wengine kutoka kwenye gari hilo lililoharibika vibaya, mahakama ilielezwa.
Lakini abiria aliyekuwa ameketi katika kiti cha mbele Ellie Tweed mwenye miaka 18, alinaswa ndani ya gari hilo lililokuwa likiwaka moto na kufa, Mahakama ya Norwich ilielezwa.
Eleanor alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela juzi baada ya kukiri kusababisha kifo kutokana na uendeshaji wake wa kizembe.
Jaji Peter Jacobs alisema: "Ulikuwa na uchovu na hukuwa na uwezo wa kuendesha gari kabisa.
"Utajutia hili kwa kipindi chote kilichobakia cha maisha yako."
Ajali hiyo ya kutisha iliyokea Novemba 11, mwaka jana kwenye Barabara ya A47 huko Runham, karibu na Great Yarmouth, Suffolk.
Eleanor, ambaye alikuwa 'akijirusha' mjini Norwich, alipata majeraha kadhaa kichwani na hana kumbukumbu yoyote ya kilichotokea.
Vipimo vimeonesha kwamba alikuwa amevuta bangi ingawa hakukuwa na uthibitisho kwamba ndivyo vilivyochangia kusababisha ajali hiyo.
Haikufahamika kilichosababisha ajali hiyo lakini abiria wengine watatu walipata majeraha makubwa na wote waliokuwa wamekaa kiti cha nyuma hakuwa wamefunga mikanda.
Barua iliyoandikwa na Eleanor, ambayo ilikabidhiwa kwa Jaji na kusomwa kwa sauti mahakamani hapo ilisema: "Najichukia mwenyewe kwa kila kitu kilichotokea na kamwe ziwezi kujisamehe mwenyewe."
Eleanor alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela na kufungiw kuendesha gari kwa kipingi cha miaka mitatu.
Pia aliamriwa kurudia mtihani wa udereva kabla ya kuruhusiwa kurejea tena barabarani.

No comments: