CHEKA TARATIBU...


Jamaa mmoja baada ya mizunguko yake ya hapa na pale, mida ya mchana kaingia hotelini kujipatia chakula cha mchana. Kama ilivyo kawaida mhudumu akamfuata na baada ya dakika kadhaa akaagiza chakula roho yake inapenda. Wakati akiendelea kula kikaingia kibabu kimoja na kibibi vikaenda kukaa meza iliyo jirani na yule jamaa. Kile kibabu kikaagiza sahani moja ya wali na maharage. Alipoletewa tu, moja kwa moja kile kibabu kikaanza kula huku kile kibibi kikimkodolea macho. Wakati wote huo yule jamaa alikuwa akifuatilia kilichokuwa kikiendelea kati ya vizee vile. Jamaa kuona chakula chao kimefikia nusu bila kile kibibi kutia mkono, akahisi kwamba hawakuna na fedha za kutosha kununua sahani mbili. Ndipo yule jamaa akaamua kumuita mhudumu na kumwamuru apeleke sahani nyingine ya wali na maharage kwa kile kibibi. Cha kushangaza kile kibibi kikainuka na kufoka, "usinidhalilishe tafadhali, sio kwamba sina fedha ila hapa namsubiria baba watoto amalize kula anipe na mimi meno." Duh, balaa!!

No comments: