Shirika
la Ugavi wa Umeme (Tanesco) mkoani hapa limetambulisha kifaa kipya ambacho ni
mbadala wa kutandaza nyaya za umeme kwa maandalizi ya kupata umeme wa shirika
hilo kwa wafugaji wa kuku pamoja na wananchi wanaojenga chumba kimoja ama
viwili.
Kifaa
hicho mbadala tayari nyaya zimesukwa ndani yake na kinajulikana kwa jina la
Readboard
(Umeta) kinauzwa na shirika hilo kinatoa unafuu wa gharama ya kutandaza nyaya kwenye nyumba na badala yake
unatumia kifaa hicho.
Katika
mahojiano na gazeti hili kwenye Maonesho ya Wakulima kwenye Uwanja wa
Nyamhong’olo,
nje kidogo ya Jiji la Mwanza, Ofisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja
mkoani
hapa, Flaviana Moshi alisema kifaa hicho cha Umeta ni mbadala wa maandalizi ya
kupokea umeme kutoka kwenye nguzo za umeme
badala ya kutandaza nyaya.
Akifafanua
alisema badala ya kutandaza nyaya ili upokee umeme kutoka kwenye nguzo wamemrahisishia mwananchi kwa
kifaa hicho cha Umeta ambacho kimeishasukwa kabisa tayari kwa matumizi ya umeme
mkubwa na mdogo.
“Tanesco
inafanya jitihada za makusudi ili kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na
huduma
hii kila sehemu ili waweze kukuza kipato chao kutokana na nishati ya umeme,”
alisema Moshi.
Alisema
kuwa Umeta ni kwa ajili ya wale ambao wamejega chumba kimoja, kwa matumizi ya
kawaida au ya kufugia kuku, baada ya kulipia gharama kisha mafundi wa Tanesco
hufika nyumbani kwa mteja kwa ajili ya kuweka na kutoa elimu ya namna ya
kukitumia.
Moshi
alisema kuwa tofauti na kuwasha taa za
ndani tu, kifaa hicho kinatumika pia
kuwashia jokofu, kupikia na kuangalia televisheni.
Alisema
hii ni mara ya kwanza kwa Tanesco kushiriki Maonesho ya Wakulima ambapo
alisema kuwa wamekuwa na manufaa sana kutokana
wafugaji wengi kujitokeza na kupata maelekezo juu ya kifaa cha Umeta.
No comments:
Post a Comment