SHULE YA TUSIIME YANG'ARA KITAIFA MATOKEO DARASA LA SABA...

Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Tusiime, Albert Katagira (kulia) akimpongeza mwanafunzi wake, Janeth Kijazi baada ya kuongoza kitaifa matokeo ya Darasa la Saba.
Wanafunzi  wa Shule ya Msingi Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam, wameongoza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka jana.
Wanafunzi kutoka shule hiyo walioshika alama za juu zaidi na kuongoza kitaifa ambazo ni 234  ni Janeth Kijazi aliyepata alama 234, Justina Kalala alama 234 na Kellen  Mudogo alama 234.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, waliofuata kwa kufanya vizuri zaidi kitaifa ni Thecla Ngewe 231 na  Stella Kagumila 230 ambao wote wanatoka katika shule hiyo ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule hiyo, Mwalimu Mkuu, Thomas Samson alisema matokeo hayo yametokana na wanafunzi kujituma na shule kuwawekea mazingira mazuri ya kusomea.
Alisema walimu wa shule hiyo ambayo imeongoza miaka minane mfululizo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi siku hadi siku ili kujua iwapo wanaendelea vizuri.
Kadhalika, katika matokeo ya Mkoa wa Dar es Salaam yaliyotolewa hivi karibuni na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando na  Ofisa Elimu wa Mkoa, Raymond Mapunda, wanafunzi kumi bora wa kike wa mkoa huo wote wanatoka Shule ya Tusiime.
Wanafunzi hao na alama zao kwenye mabano ni Janeth Kijazi (234), Justina Kalalaa(234), Kellen Mudogo (234), Thecla Ngewe (231), Stella Kagumila (230), Asia Komba (229), Grace Nyondo (226), Praise Bagenda (226), Lisa Magoti (225) na Najima Majid aliyepata alama 224.
Kumi bora waliofanya vizuri kwa upande wa wavulana ni Jimmy Luhomvya 233 (Tusiime), Dule Mutagwaba 231 (Tusiime), Fray Seyumwe 231 (Tusiime), Maximillian Machage 229 wa Moga Kinondoni,  Saad Mussa 229 (Tusiime), Gerald Kasamala 229 (Tusiime), Gift Kilupa 229 (Tusiime).
Wengine ni Joel Mutagwaba 228 (Tusiime), Shaban Kawaia 227 (Mtoni Temeke) na Alfred Shami wa Shule ya Msingi Mlimani.

No comments: