MWALIMU WA KIKE AKABILIWA NA KIFUNGO KWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE


Mwalimu Cox alipokuwa akitoka mahakamani.

Mwalimu wa kike ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 16 ametahadharishwa kwamba anakabiliwa na adahabu ya kifungo jela baada ya mahakama kuelezwa kwamba alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtoto huyo kwa kipindi cha miezi sita.

Lauren Cox, miaka 27, alikuwa akifundisha kwenye shule moja kusini mwa London, ndipo alipojitumbukiza katika mahusiano na kijana huyo, ambaye hakutajwa kwa sababu za kisheria.
Alipandishwa katika Mahakama ya Croydon, ambako alikiri mashitaka matano yanayohusiana na mahusiano ya kimapenzi na kijana mwenye umri wa kati ya miaka 13 na 17 wakati akiwa katika dhamana yake.
Mashitaka hayo ni pamoja na kugusa kwa dhamira ya kufanya mapenzi mnamo Machi 9 na Machi 16 mwaka jana na pia kufanya mapenzi kati ya Aprili na Septemba 2015 wakati akiwa na umri wa miaka 26 na kijana huyo akiwa na miaka 16 tu.
Cox alikamatwa Septemba 16, 2015 baada ya wanafunzi kuwaeleza wazazi wake kuhusu kilichokuwa kikiendelea kati ya wawili hao.
Kisha baadaye wakawasiliana na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye aliwasiliana moja kwa moja na Ustawi wa Jamii.
Cox alikutana kwa mara ya kwanza na kijana huyo wakati akiwa na miaka 13, na mwathirika huyo alisema wakaunda mahusiano ya karibu.
Kwa mujibu wa polisi, mwalimu huyo akaanza mahusiano ya kimapenzi na kijana huyo mnamo Januari 2015.
Mwendesha Mashitaka Brian Reece, aliieleza mahakama hiyo; “Tofauti ya umri ni miaka 10 pekee hivyo hii ni mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi.”
Cox na kijana huyo walikuwa wakikutana baada ya muda wa masomo na wakati wa likizo. Mwalimu huyo alikuwa akimtumia picha za kimahaba na video alizojirekodi mwenyewe na kumtumia kijana huyo.
Lakini kijana huyo alisitisha mahusiano hayo Agosti 2015 baada ya wazazi wake kutilia mashaka kilichokuwa kikiendelea na kumkabili kijana wao ambaye alikiri kuwa na mahusiano na Cox.
Hatahivyo, Cox aliendelea kumtumia kijana huyo meseji zilizowafanya wazazi wa kijana huyo kuripoti kwa vyombo husika.
Cox, mwalimu wa masomo ya biashara, ambaye aliwasili mahakamani hapo akiwa amevalia suruali nyeusi, koti, na miwani alinyamaza kimya kizimbani wakati akisomewa mashitaka yote matano anayokabiliwa nayo.
Cox, mkazi wa Oxted mjini Surrey, alipatiwa dhamana na anatarajiwa kurejea mahakamani hapo mwezi ujao kwa ajili ya hukumu.
Alipatia dhamana hiyo kwa masharti ya kutoonana na kijana huyo au kufika shuleni hapo.

No comments: