MTOTO WA MIEZI MITANO ANYOFOLEWA ‘KICHWA CHA PILI’ BAADA YA WAZAZI KURIDHIA UPASUAJI HATARI WA ASILIMIA 50/50Mtoto aliyekuwa na uvimbe unaoonekana kama kichwa cha pili amenusurika kifo katika upasuaji wenye hatari kubwa uliodumu kwa masaa sita kuondoa uvimbe huo mkubwa, ambao madaktari awali walisema hauwezi kutibika.

Yamanoor Naranal, ambaye ana umri wa miezi mitano tu, alizaliwa nchini India akiwa na matatizo hayo – hali inayotokea kwa nadra mno ambapo majimaji ya ubongo yanatiririka nje ya fuvu la kichwa.
Wazazi Karriappa Naranal, miaka 35, na mkewe Shridevi Naranal, miaka 28, kutoka kijiji cha Tavariyara, kilichopo jimbo lililoko kusini kwa Karnataka, walielezwa kwamba hakuna matarajio ya kutibika muda mfupi baada ya mtoto wao kuzaliwa.
Wanandoa hao waliochanganyikiwa walifika kwenye hospitali hiyo ya serikali mara kadhaa wakijaribu kutafuta msaada, lakini baada kuwa wameshakata tama ya mtoto wao huyo wa kiume kuweza kupatiwa matibabu.
Pale mhudumu wa afya akashauri wazazi hao kumpeleka Yamanoor kwenye hospitali bora zaidi mjini Bangalore wazaiz hao wakaitumia fursa hiyo – ambayo ilipelekea uondoshwaji wa uvimbe huo kimiujiza kufuatia upasuaji hatari.
Mr Naranal, ambaye anafanya kazi kama kibarua wa ujenzi na kulipwa takribani Dola 2 za Kimarekani (Karibu Shilingi 5,000 za Kitanzania) kwa siku, alisema: “Madaktari wengi walinieleza kulikuwa na asilimia 90 za mtoto wangu kufa endapo angefanyiwa upasuaji. Madaktari walisema sikutakiwa kuhatarisha sababu upasuaji wa mafanikio hautowezekana.
“Lakini tukapata mwanga wa matumaini mjini Bangalore pale daktari mmoja aliposema kuna nafasi ya asilimia 50 ya kupona ndipo tukakubali ifanyike.”
Yamanoor akatibiwa katika Hospitali ya Sapthagiri, mjini Bangalore, mwezi uliopita, na baada ya upasuaji uliochukua masaa sita madaktari wakaondosha kwa mafanikio uvimbe huo, ambao ulikuwa na ukubwa wa takribani mzingo wa kipenyo cha sentimeta 20.
Dk Hariprakash Chakravarthy, bingwa wa upasuaji katika hospitali hiyo, alisema: “Hali hii hutokea kwa mama ambao wana upungufu wa asidi ya foliki.
“Tatizo hili hufaamika kama occipital encephalocele, na hutokea pale kunapokuwa na uwazi kati ya mifupa miwili ya fuvu, na fuvu linapoendelea unaendelea na kuwa uvimbe uliojaa kimiminika.
“Tulikuwa na matarijio finyu mno kuhusu kufanikiwa kwa upasuaji huu kuzingatia ukweli kwamba mtoto mdogo hawezi kumudu kupoteza kiasi kikubwa cha damu.
“Hata upotevu wa mililita 10 hadi 20 za damu unaweza kusababisha moyo kusimama kufanya kazi. Tunapokata sehemu ya ubongo husababisha upotevu wa kiasi fulani cha damu lakini tunashukuru hakuna chochote kibaya kilichotokea na mtoto huyu mdogo yu hai.”
Mtoto huyo wa kiume aliruhusiwa kutoka hospitalini mwishoni mwa wiki iliyopita – takribani mwezi mmoja baada ya matibabu yake – na sasa anaendelea kujiuguza nyumbani.
Lakini atatakiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwezi ujao na kufanyiwa uangalizi wa mara kwa mara, kila baada ya miezi mitatu.
Bw Naranal aliwashukuru madaktari kwa kumfanyia upasuaji mtoto wake na kusema: “Sasa anaendelea vizuri, namshukuru sana yule mhudumu wa afya. Mtoto wangu atatakiwa kuangaliwa afya yake kila baada ya miezi mitatu lakini yote ni heri.
“Siwezi kuamini simulizi yake ina mwisho wenye furaha. Ninamshukuru Mungu na madaktari hawa.”

No comments: