Msichana mwenye umri wa miaka 15 amekamatwa kwa tuhuma za
kumuua mama yake mzazi na rafiki wa kiume wa mama huyo kwa kile alichodai
kubakwa na mwanaume huyo, polisi wamesema.
Binti huyo, ambaye hajatajwa jina, alidaiwa kumweleza mama
yake kuhusu shambulio alilofanyiwa, lakini mama huyo akagoma kuamini madai
hayo, vyanzo vya kipolisi vilisema.
Akiwa amechukizwa na uamuzi wa mama yake, askari wamesema
msichana huyo akamfyatulia risasi mama yake huku rafiki wa binti huyo akimuua
rafiki wa kiume wa mama huyo, Desemba 27, kabla ya binti huyo kutorokea
nyumbani kwa binamu yake.
Kwa mujibu wa maofisa, msichana huyo amekuwa akiishi na ndugu yake huyo bila
kubainisha kwamba alifanya tukio hilo mpaka hivi leo alipoweka bayana.
Askari walisema binamu yake huyo alikuja kufahamu baada ya
ukimya wa siku kadhaa kutoka kwa wazazi wa binti huyo, ndipo binti huyo akakiri
kuhusika na kilichotokea.
Maofisa wa polisi ndipo walipokwenda nyumbani kwa familia ya
binti huyo iliyoko ghorofa ya tano ya jingo moja lililoko kwenye majengo ya
Sheepshead Bay Houses na kukuta mabaki ya miili ya mwanaume na mwanamke.
Ingawa awali wachunguzi walidhani waathirika hao walichomwa
na vitu vyenye ncha kali, polisi walibaini baadaye kitu tofauti.
No comments:
Post a Comment