Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es
Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, anatarajiwa kuongoza misa ya Ijumaa
Kuu, itakayofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jimboni humo.
Wakristo wote duniani hufanya misa hiyo kila
mwaka, kukumbuka mateso na kufa kwa Yesu Kristo.
Ratiba iliyotolewa Dar es Salaam jana na
Katibu wa Jimbo, Dennis Wigirwa ilionesha kuwa Pengo ataadhimisha misa hiyo
kanisani hapo itakayoanza saa 9:00 jioni.
Pia, alisema kuwa Misa ya mkesha wa
sikukuu ya Pasaka, itafanyika saa 2 usiku Jumamosi na Askofu huyo ndio atakayeiongoza.
Aliongeza kuwa misa ya Pasaka ya kukumbuka
kufufuka kwa Yesu Kristo. itafanyika saa 3:00 asubuhi na itaongozwa na Pengo.
No comments:
Post a Comment