CHEKA TARATIBU: LAZIMA NIMEFAULU MTIHANI

Asubuhi moja wanafunzi wapo darasani wakimsikiliza mwalimu wa somo ya Hisabati aliyekuwa akijiandaa kugawa mitihani ya somo lake. Kati yao alikuwapo Nonda, mwanafunzi ambaye mara zote amekuwa akishika mkia katika darasa hilo.
Ndipo mwalimu alipoanza kuita majina ya wanafunzi akianzia na yule aliyepata alama za chini kabisa kuelekea aliyeshika nafasi ya kwanza. Baada ya kuita takribani majina ya wanafunzi 50, ndipo Nonda alipoanza kutabasamu akiamini safari hii amefanya vizuri kwani mwalimu alishafikia aliyepata alama 70%. Kichwani akawa amejihakikishia kwamba kama hajapata 100% basi walau 85% hawezi kukosa. Mwalimu akaendelea kusoma majina mpaka walipobaki wanafunzi wawili ambao hawajapata majibu yao, ambao ni Nonda na Duma ambaye kila mara amekuwa akishika nafasi ya kwanza. Nonda akazidi kujipa matumaini kwamba safari hii ataibuka kidedea. Mwalimu akasema, "Hapa nimebakiwa na matokeo ya wanafunzi wawili, Duma aliyepata alama 100% na mpuuzi mmoja ambaye kapata 0% na hakuandika jina!! Duh...

No comments: