MKATABA UKARABATI UWANJA WA NDEGE KIA WASAINIWA


Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa ukarabati wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) na majengo ya uwanja huo na kampuni ya ujenzi ya  kimataifa ya Uholanzi, iliyoshinda tenda ya kufanya kazi hiyo  ndani ya miezi 23.

Mkataba huo ulisainiwa mwishoni mwa wiki na Meneja wa kampuni  hiyo, Erick Van Zuthem na mwenzake, Harko Kloeze ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Afrika na Afrika ya Kati.
Kwa upande wa Tanzania, mkataba huo ulisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO na Christopher Mkoma, ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ufundi wa uwanja huo.
Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Mkoma alisema kuwa wanatarajia kutumia Euro milioni 37, sawa na zaidi ya Sh bilioni 70.
Alisema katika ukarabati huo utafanyika kwa wakati uliopangwa na bila kuharibu safari za ndege.
"Uwanja huu ulijengwa na Mwalimu tangu mwaka 1971 tangu wakati huo hadi leo haujawahi kukarabatiwa tena, hivyo unahitaji matengenezo makubwa ambayo yatakwenda sambamba na kuongeza miundombinu ya maji safi na salama ili yaweze kuwa ya uhakika na mengi kulingana na mahitaji ya uwanja huo," alisema.
Alisema maji yanahitajika kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kuhakikisha magari ya zimamoto hayakosi maji kwa usalama wa ndege zinazotua na kuruka.  Mbali na ndege za kawaida, kwa siku ndege 12 za kimataifa hutua.

No comments: