MABEHEWA MAPYA TRL KUANZA KAZI APRILI MOSI

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imesema mabehewa 15 kati ya 22 ya abiria yaliyonunuliwa na serikali kutoka Korea Kusini yataanza kutoa huduma kwenda Kigoma kupitia stesheni 17 kuanzia Aprili mosi mwaka huu.

Imesema mabehewa mengine yatabakia, ikiwa ni kwa sababu za kiuendeshaji ndani ya kampuni hiyo.
Kaimu Mkuu wa Masoko wa TRL, Charles  Ndenge alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza  kuwa mabehewa hayo yalishafanyiwa majaribio na  kampuni hiyo na kuridhika kuwa hayana kasoro. Aidha Mamlaka ya Usafiri wa  Nchi Kavu na Majini  (Sumatra) imetoa idhini ya kuanzishwa kwa huduma hiyo kwa kuyatumia mabehewa hayo baada ya kutimizwa kwa masharti ya uendeshaji. Alisema safari za treni zitakuwa mara moja siku za Jumapili ikianzia stesheni ya Dar es Salaam.

No comments: