Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Warioba amevitaka vyama vya siasa kuzingatia matakwa ya
wananchi katika suala zima la Kura ya Maoni
ya Katiba Inayopendekezwa na badala ya kuwagawa.
Aidha, Warioba amesema anaamini baadhi ya
vipengele vilivyokataliwa katika Rasimu ya Katiba, ipo siku vitafanyiwa kazi kuondoa migongano huku
akisisitiza, kisheria kura ya maoni siyo
mwisho wa mchakato.
Warioba alisema kwa sasa,
badala ya kuwaweka wananchi
pamoja na kukubaliana wanachotaka , upo mvutano huku wengine wakitaka
Katiba Iliyopendekezwa ikubaliwe na wengine wakitaka wananchi waikatae.
“Kwa suala hili la kundi la Ukawa kuwasihi
wafuasi wake kutoshiriki katika upigaji kura ya maoni, inaonyesha dhahiri
hakuna maridhiano na wananchi kwani badala ya kujua matakwa yao, vyama vya siasa vinawagawa wananchi katika
suala hilo jambo ambalo linaonyesha vyama hivyo vinajitazama vyenyewe,”
alisema.
Alikuwa akizungumza katika kipindi cha Dakika
45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV.
Alisema suala la kupiga kura ya maoni ni
kuangalia maridhiano na wananchi na si vyama vya siasa. Alisema hata katika
mchakato wa awali, waliangalia
maridhiano ya wananchi na walihakikisha
maoni yao yanaingia kwenye Katiba pendekezwa.
Alisema vyama vya siasa vinataka maridhiano
yao bila kuangalia matakwa ya wananchi
na kukubaliana jambo, alilosema ni tatizo.
Alisisitiza kwamba anaamini baadhi ya
vipengele vilivyokataliwa, ipo siku vitafanyiwa kazi kuondoa migongano.
Alisema katika Katiba Inayopendekezwa, suala
la mgawanyo wa madaraka halijaainishwa lakini anavyoona maendeleo katika
dunia na matatizo, ipo siku lazima
madaraka yatenganishwe, kwani kutakuwa na migongano kati ya Serikali na Bunge.
Alisema ingawa masuala hayo hayajaingizwa
katika Katiba Inayopendekezwa, kama ilivyokuwa kwenye rasimu iliyoandaliwa na
Tume aliyokuwa akiiongoza, anaamini
kutakuwa na mabadiliko kabla ya kura ya maoni au baada kwa kuwa hayaepukiki.
“Matatizo haya ya wazi ya masuala kama ya
mgongano wa madaraka na Muungano yatafanywa kabla au baada ya kura ya maoni
kwani kuna mambo katika Katiba pendekezwa hayawezi kutekelezwa na
hayazungumziki,” alisema.
Akizungumzia suala la maadili,Warioba alisema
sheria ya maadili ipo, lakini haina nguvu kama ilivyokuwa kwa nchi
nyingine. Alitoa mfano wa Ufilipino
akisema walikuwa na sheria hiyo lakini wakaweka kwenye katiba iwe rahisi
kutekelezwa. Alitaja pia Namibia na
Kenya.
Alisema suala la mgawanyo wa madaraka bado ni
muhimu kwani kwa kutenganisha, kunaweza kusaidia katika uwajibikaji . Alitoa
mfano wa sakata la Tegeta Escrow bungeni
na kusema Bunge na Serikali ziliingiliana madaraka badala ya serikali kuwa na kauli moja.
“Hebu angalia suala la Bunge kumfukuza Katibu
Mkuu, hii siyo kazi yake, lilichanganya madaraka, kama Bunge haliridhiki na
mwenendo wa serikali haliwezi kwenda kufukuza watumishi wa serikali. Bunge
linatakiwa kusema kutokuwa na imani na serikali na siyo kufurahia kusema fulani
afukuzwe. Siyo utaratibu mzuri,” alisema.
Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kazi ya Bunge
ni kusimamia serikali na siyo kufukuza watu, kwani wakati mwingine kunakuwa na
suala la visasi na kufukuza watumishi ambao hawahusiki.
Kuhusu Muungano, alisema, “Hili jambo ni ‘serious’(nyeti) lazima kufika
wakati kuwa na nchi moja na hata kuangalia jinsi ya kuweka sawa suala la muundo
wa serikali.”
Alisisitiza
msimamo wake kwamba yeye ni muumini wa Muundo wa serikali mbili kwenda
moja na siyo muumini wa serikali tatu. Alipendekeza kwenda hatua kwa hatua hata
baada ya miaka 100 kupata serikali moja.
Warioba alisema siku ya
kupiga kura ya maoni, inaweza kubadilishwa kwani haiko kisheria na
haitaathiri mchakato wa kupata Katiba mpya.
Alisema tarehe ya kupiga kura, imewekwa na
wanaohusika na inaweza kuahirishwa kwa kadri wanavyoona maandalizi yamekamilika
katika kuandikishwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
8 comments:
Undeniably believe that which you said. Your favorite justification appearedd to be on the net the easiest thing to be aware of.
I say to you, I definitely get irked while people consideer worries tjat
they plainly don't know about. You managed to hit the nail upon the topp and defined out the whole
thing without having side effect , people can take a signal.
Will likely be back to get more. Thanks
Can you tell us more about this? I'd like to find out more details.
Simplу desire to saү yоur article is as astounding.
The clarity in your ost is just excellent and i can asѕume
you're an expert on this suƅject. Fine with уour permission let mme to grab y᧐ur fеed to
keep upp to dаte with forthcoming ρost. Thаnks a milliߋn and
pleаse carry оnn the rewarding work.
I loved ɑѕ mudh ɑs you'll receive carried
out right hегe. The skegch iss tasteful, your authored subject
matter stylish. nonetһeless, уou command gеt bought an impatience ovеr that ʏⲟu wish be delivering
the fⲟllowing. unwell unquestionably come fuгther formеrly agaіn as exаctly the same nearly vewry often іnside cas you shiwld tһis hike.
Remarkable issues һere. I'm νery happy to see your article.
Thɑnks a lot ɑnd I am taking a lokok forward tօ touch
you. Will you kindly drop me а mail?
Hmm it looks ⅼike youг website ate my first comment (it waѕ super long) so
Ӏ guess I'll ϳust sum іt uр what I submitted and say, I'm thorougһly enjoying yoᥙr blog.І too am an aspiring blog
writer but І'm stiⅼl neᴡ tоo everything.
Ꭰo уou haᴠe any helpful hints for inexperienced blog writers?
І'd certainly aрpreciate іt.
What's uup everүone, іt'ѕ my first pay а quick visit at
thyis website, and post iѕ in fact fruitful designed
f᧐r me, қeep up posting theѕе types оf posts.
Υоur style is reɑlly unique іn comparison to otheг
people I've read stuff from. Ӏ appreciate you for posting ᴡhen yoս've
got the opportunity, Guess I wіll ϳust book
mark tһis web site.
Post a Comment