SUMATRA YAZUIA VYOMBO VYA USAFIRI WA MAJINI


Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imevizuia kutoa huduma kwa muda usiojulikana vyombo vyote vya usafirishaji wa majini vya mkoani hapa hadi hapo vitakapokaguliwa.
Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga, Walukani Luhamba ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha pamoja na maofisa uvuvi na askari wa majini kilichofanyika jijini humo jana.
Alisema kuna umuhimu wa kisheria kwa vyombo vyote vya usafiri kuhakikisha vinakaguliwa na maofisa wa Sumatra ili kuhakikisha ubora na usalama safarini.
“Kutokana na ongezeko la ajali za baharini, Sumatra kuanzia sasa hapa mkoani tumeamua kuvihakiki upya ili tuweze kujiridhisha kwamba vyombo vyote vinavyotumika kusafirisha abiria au mizigo vinakuwa kwenye hali ya ubora na usalama unaostahili kabla ya safari,” alisema.
Luhamba alisema pamoja na kwamba vyombo hivyo vilishasajiliwa kufanya shughuli za usafirishaji abiria na uchukuzi wa mizigo mbalimbali lakini kigezo hicho hakitoshelezi kuridhia kwamba viko katika usalama unaohitajika safarini.

No comments: