Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema wanaobeza uwezo wake kiutendaji
baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo, wasubiri waone
atakavyokuwa.
Aidha,
ameweka wazi kile anachoamini anashutumiwa na kubezwa na watu kuhusu uteuzi huo
na kusema wanaofanya hivyo, wanafahamu kwamba masuala yao kadhaa ndani ya
wilaya hiyo yanayokwenda kinyume na taratibu, hayatafanikiwa.
Akiendelea
kujibu wanaoshutumu uteuzi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya
habari, alisema kwa sasa hawezi kutoa ahadi ni nini atafanya isipokuwa, anasubiri kuingia ofisini.
Akihojiwa
katika kipindi cha asubuhi cha Redio ya Clouds, alisema pia anamsikiliza Rais
atakachomwambia afanye kwa kuwa yeye ni mwakilishi wake wilayani humo.
Akizungumzia
kuhusu taarifa za kupata nafasi hiyo
kuwa gumzo katika jiji kuliko wakuu wengine wa wilaya, alisema inaonesha ni kwa
jinsi gani watu wanatambua utendaji wake.
Alisema
alipata taarifa za uteuzi huo wakati
akitoa mada katika kikao cha kazi cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) na kushangaa watu wakipeana taarifa.
“Kuna
watu wanabeza uteuzi wangu kwa kuonekana nimepewa wilaya kubwa. Nataka
kuwaambia wasubiri waone tu,” alisema na kutaka Watanzania kuacha tabia ya
kumjadili mtu au jambo bila kufahamu vizuri.
Alisisitiza
kuwa Watanzania wamekuwa na tabia ya kushabikia jambo wasilolijua au mtu
wasiyemjua kwa kufuata mkumbo; jambo ambalo siyo zuri ni vyema kufahamu kwanza
ndipo uweze kusema.
Akizungumzia
baadhi ya vyombo vya habari vilivyotoa
taarifa za uteuzi wake kwa kumdhihaki, alisema wamefanya hivyo kwa
maslahi yao ya kuuza.
Pia
alielezea uteuzi wake umekuwa gumzo, kutokana na uwezo wake wa kazi katika
UVCCM pamoja na uwezo wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Uteuzi
wa Makonda ambao umefanywa na Rais Kikwete, unaonesha kuwashitua wengi; hali
ambayo imefanya watu wengi kumbeza hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi
ya wanaobeza, wanadai kwamba Makonda hana sifa ya kuongoza wilaya kubwa kama
Kinondoni, ambayo ina changamoto na migogoro mingi ya ardhi.
Makonda
ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina lake limekuwa
kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kushiriki kuvuruga mdahalo ulioandaliwa
na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, tuhuma alizokanusha.
Pia,
kujitokeza kwake hadharani kumpinga mmoja wa watu wanaotajwa kuwania urais,
kuliongeza jina hilo kuwa maarufu.
Maisha
ya Makonda pia ambaye baada ya kushindwa
Umakamu Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM, alitoa shutuma kuhusu uchaguzi huo na baadaye alirejeshwa
ndani ya umoja huo kwa kupewa nafasi anayoshikilia sasa ya ukatibu wa uchipukizi
na uhamasishaji.
Katika
hatua nyingine, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Amon
Mpanju amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo mpya wa wakuu wa wilaya
kwa mamlaka aliyonayo.
Hata
hivyo, alidai anasikitishwa na kukosekana kwa mwakilishi wa watu wenye ulemavu
katika wadhifa huo.
Alisema
ni wakati sasa kwa watu wenye ulemavu
wapatiwe fursa kuonesha uwezo.
‘Kati
ya walioteuliwa hakuna mtu mwenye ulemavu, jamii ya watu wenye ulemavu kilio
chetu ni ushirikishwaji katika ngazi za maamuzi. Mtu asiyeona au mwenye tatizo
la ngozi au asiyeweza kutembea, haimaanishi kuwa hana uwezo wa kufikiri na kuwa
kiongozi bora la hasha,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment