Jumapili moja Mchagga kaingia
kanisani kusali baada ya pilika za wiki nzima. Dakika chache likapitishwa kapu
kwa ajili ya kutoa sadaka. Ilipofika zamu ya Mchagga, akachomoa noti ya
Shilingi 500 na kuingiza kwenye kapu kwa kificho bila kuonekana na mtu yeyote
jirani yake.
Baada ya dakika 15 hivi, Mchagga
akahisi kuna mtu anamgusa begani kutokea benchi la nyuma yake. Akageuka na
kumwona mzee mmoja wa makamo akimkabidhi noti mbili za Shilingi 10,000! Bila
kusumbua akili, Mchagga akajua fika mzee yule anataka asaidiwe kuweka sadaka.
Akapokea na kuzitumbukiza ndani ya
kapu. Baada ya misa kumalizika, Mchagga akamwendea yule mzee na kumpongeza,
“Aisee, tunataka waumini kama wewe wenye moyo huo, yaani umechangia Shilingi
20,000! Sio jambo dogo mzee wangu, Mungu akubariki.”
Mzee akajibu, “Hapana, sijachangia
mimi. Wakati unatoa sadaka yako mfukoni ndipo ukadondosha zile pesa.
Nilichofanya ni kuziokota na kukurejeshea.” Kusikia vile Mchagga akamkimbilia
Padri kuomba arejeshewe pesa zake, lakini akakataliwa kwa maelezo kwamba
zimeshakabidhiwa kwa Mungu. Palepale akaanguka na kupoteza fahamu.
Alipozinduka akakutana uso kwa uso
na mwanamke aliyevalia gauni jeupe. Mchagga akasema, “Afadhali nimekuona
malaika, naomba umwambie Mungu anirejeshee zile pesa zangu!” Yule mwanamke
akamjibu, “Mie sio malaika bali ni nesi. Walikuleta hapa hospitali ukiwa
hujitambui!” Kusikia vile Mchagga akanguka na kupoteza tena fahamu…
No comments:
Post a Comment