BREAKING NEWS!!! MTOTO ALBINO ALIYETEKWA AOKOTWA AKIWA AMEKUFA MSITUNIMwili wa mtoto Yojana Bahati (1) ambaye ana ulemavu wa ngozi (albino) umeokotwa msituni katika kijiji cha Ilelema.

Mtoto huyo alitekwa nyara juzi nyakati za usiku na watu wasiojulikana mkoani Geita baada ya kumvamia nyumbani kwao akiwa amelala na mama yake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukiwa umefukiwa kwenye shamba moja kijijini humo huku mikono na miguu yake ikiwa imekatwa na kunyofolewa.
Inasemekana wanakijiji wa Ilelema wamekuwa wakikimbia huku na huko kujificha kwa kile kinachoaminika hofu ya kukamatwa na vyombo vya dola kuhusiana na tukio hilo.
Taarifa za polisi zinasema kwamba tayari mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba anashikiliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Katika tukio la kutekwa mtoto huyo, mama wa albino huyo Ester (30) alijeruhiwa kwa kukatwakatwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kisha watu hao kutokomea kusikojulikana. 

No comments: