Mtu mmoja ameuawa na mwingine kujeruhiwa katika matukio mawili
tofauti ya uhalifu yaliyotokea wilaya Bunda hivi karibuni.
Mfanyabiashara wa samaki aliyeuawa kwa kupigwa risasi ni
Mkome Marwa (39) mkazi wa mtaa wa Nyasura mjini Bunda.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Philipo Kalangi, tukio hilo ni la Januari 12 mwaka huu saa 3:00 usiku katika
eneo la Nyasura, mjini Bunda.
Marwa alikuwa na
mkewe wakirejea nyumbani kwao kabla ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Kilangi alisema
mauaji hayo, yana utata kwa kuwa walioua hawakuchukua chochote.
Katika tukio
lingine la usiku huo wa Januari 12, saa
4:00 eneo la Bunda Day, Ndaro Malemi
(25), alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na
mtu asiyefahamika ambaye pia hakuchukua kitu chochote.
Akisimulia mkasa
huo majeruhi huyo akiwa katika hospitali
ya DDH-Bunda, alisema kuwa mwanamume huyo aliyekuwa amevaa koti jeusi,
alimvizia njiani na kumwamuru atoe kila kitu.
Alisema kwamba alipojaribu kukimbia, ndipo mtu huyo alimpiga
risasi mbili na kisha akatokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu chochote.
No comments:
Post a Comment