ALIYELAWITI MTOTO WA MIAKA SITA ATUPWA JELA

Mfanyakazi wa nyumbani, Hatibu Adamu (20) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kike wa miaka sita.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Said Mkasiwa alisema kuwa upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano na kwamba mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa. 
Awali, Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto alidai mahakamani hapo kwamba kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji nchini, mshitakiwa huyo apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
Kabla ya hukumu hiyo, Adamu alidai kwamba anasumbuliwa na vidonda vya tumbo hivyo aliomba apunguziwe adhabu. Hata hivyo mahakama hiyo haikusikiliza maombi hayo. 
Mshitakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Majohe, Dar es Salaam, alidaiwa kwamba tarehe isiyofahamika Septemba, mwaka jana, maeneo ya Majohe Wilaya ya Ilala, Adamu alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka sita huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

No comments: