NHIF YAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KWA KUHAMASISHA CHF


Viongozi wa dini mkoani Tabora wametoa mchango mkubwa katika kuhamasisha waumini wao kujiunga na Mfuko wa Afya wa Jamii(CHF) na kuufanya mkoa huo kuwa katika hali nzuri ya watu wake kupata matibabu.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Magharibi-Tabora Emmanuel Adina katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Kitaifa mjiniTabora.
Adina imeongeza kuwa viongozi wa dini zote wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha waumini wao kujiungana CHF ilikuwa na uhakika wa kupata huduma stahiki ya matibabu.
Aidha amesema kuwa viongozi hao wamekuwa wa kihamasisha watu wao misikitini, kwa upande wa Waislam na makanisani kwa Wakristo. Hadi sasa jumla ya kaya 38,000 wamejiunga na Mfuko huo huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 30 ya waliojiungana CHF ifikapo Juni 2015,
Meneja huyo ameitaja wilaya ya Igunga kuongoza katika uhamasishaji wa wananchi kujiungana CHF. 

Adina amezitaja wilaya nyingine ambazo kaya nyingi zimejiunga na Mfuko huo kuwa ni Nzega, Uyui, Urambo na Sikonge.
Katika wilaya hizo kinachosaidia zaidi watu kujiunga ni kuwepo wilayani humo vyama vya ushirika vya msingi vya tumbaku.

No comments: