BINTI WA MBUNGE WA TEMEKE ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2014Siti, binti wa Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania  (Redd’s Miss Tanzania 2014) katika shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mlimbwende huyo, ambaye kablaya kutwaa taji hilo alitawazwa kuwa Miss Temeke, aliwabwaga warembo wengine 30 waliokuwa wakiwania taji hilo mwaka huu.
Kwa ushindi huo, Siti amejinyakulia kitita cha Shilingi milioni 18, ambapo ukumbini hapo alikabidhiwa hundi ya thamani ya Shilingi milioni 10 kwa maelezo kwamba kiasi kilichobaki cha Shilingi milioni 8 atakabidhiwa baada ya shindano hilo.
Siti ataiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Miss World mwakani, ambapo mwaka huu Tanzania itawakilishwa na mshindi wa mwaka jana, Happiness Watimanywa kutoka Dodoma.

No comments: