TAARIFA ZA HIVI PUNDE AJALI YA BASI LILILODAIWA KUUA 48

Taarifa tulizopata hivi punde kuhusiana na habari za kupinduka kwa basi ambapo ilisemekana abiria 48 walipoteza maisha mapema leo ni kwamba watu wanne tu ndio waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Air Bus lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Tabora ambapo lilipofika eneo la Berega, Gairo ndipo likapinduka.

No comments: