MADAWATI YAFUNGIWA GHALANI WANAFUNZI WAKISOTA SAKAFUNI


Madawati yamefungiwa kwenye ghala huku wanafunzi wanakaa chini kwenye shule ya msingi ya Kijiji cha Nyanyanje katika Manispaa ya Lindi mwaka huu, mkoani hapa. 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Lindi. 
Alisema pamoja na habari ya madawati kuwa ghalani lakini pia kuna mabweni katika Shule ya Sekondari ya Ng'apa yanayotakiwa wanafunzi 70 lakini waliopo ni chini ya kiasi hicho. 
Mwananzila alisema kuwa kuna umuhimu uongozi wa Manispaa ufanye jitahada za makusudi ili kuweza kujaza nafasi za mabweni ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wa kike ambao wanakatisha masomo yao kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wakati wakirudi nyumbani au kwenda shuleni. 
Hata hivyo alisema kuwa pamoja kuwa Manispaa ilipatiwa hati safi ya msisitizo, lakini kuna deni la Sh milioni 137.7 kwa kipindi cha 2012/2013. 
Alisema fedha hizo zingekusanywa zingeweza kufanya kazi za kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi. 
Aidha alisema kwamba halmashauri hiyo inadaiwa na wadau mbalimbali Sh milioni 202 hayajalipwa na mamlaka hiyo, kwa hiyo ifanyike jitihada kulipa deni.

No comments: