HATIMAYE KIMEELEWEKA WAFANYAKAZI TAZARA


Wafanyakazi  wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)  wamelipwa mishahara yao ya miezi minne waliyokuwa wakidai . 
Hatua hiyo imemaliza mgogoro uliodumu muda mrefu kati ya mamlaka hiyo na wafanyakazi. 
Tangu  Aprili hadi Agosti mwaka huu , wafanyakazi hao walikuwa katika mgogoro na Tazara wakishinikiza kulipwa fedha zao, hatua ambayo ilisababisha kutishia kugomea kazi mara kwa mara. 
Katibu wa  Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU) Elasto Kiwele, alimwambia mwandishi jana kwamba mishahara hiyo imelipwa na kubakia madai ya Agosti ambayo  hayakuwepo katika madai hayo ya awali. 
“Malipo yaliyotolewa ni kwa ajili ya miezi ya Aprili, Mei, Juni na Julai, deni lililobaki ni la  mwezi ulioisha ambao hata hivyo kimsingi suala lake halikuwepo katika madai tuliyokuwa tukiyalalamikia,” alisema Kiwele. 
Katibu huyo wa Trawu aliitaka Menejimenti ya Tazara kuweka mipango mizuri ya  utendaji kazi ili kuwawezesha wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ya uzalishaji na hivyo kuongeza ufanisi wa mamlaka hiyo.

No comments: