CHADEMA WAANZA MKUTANO MKUU


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana kilianza mkutano mkuu wa chama hicho ambapo Baraza la   Wazee wa chama hicho lilichagua viongozi wake. 
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza hilo anayemaliza muda wake, Nyangaki Shilungushela aliwataka wazee kushikamana na kusaidia ujenzi wa taifa kwani wazee ni hazina ya busara. 
Alisema kupitia mkutano huo ambao pia unachagua viongozi wapya wa baraza hilo, aliwataka wajumbe kuchagua kwa haki na wasifuate mkumbo kwani chama kinahitaji wazee wenye uwezo wa kusaidia ujenzi wa taifa. 
Awali akitoa salamu za chama hicho, Katibu Mkuu wa Chadema  Willbrod Slaa aliwapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa kuitikia mwito wa kushiriki kwenye mkutano huo. 
Slaa aliwashauri kuwa ni vyema kuchagua viongozi kwa uhuru na kamwe wasikubali kurubuniwa kwa kupewa rushwa, kwani kufanya hivyo kutasababisha kupatikana kwa viongozi wa wazee wasioweza kusaidia taifa wala chama. 
Mkutano wa chama hicho unaendelea leo na utamalizika Septemba 16, mwaka huu.

No comments: