ASKOFU KEZAKUBI KUONGOZA TENA KANISA NA AICT


Askofu Silas Kezakubi, amechaguliwa tena kuliongoza Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwa kipindi kingine cha miaka minne. 
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo, Askofu Kezakubi ambaye  ni Askofu wa  AICT Dayosisi  ya Tabora alishika tena wadhifa huo baada ya kupata kura 511 kati ya kura 685 zilizopigwa na  wajumbe wa mkutano mkuu wa kanisa hilo nchini. 
Katika uchaguzi huo, Askofu Musa Magwesela Dayosisi ya Geita alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu Msaidizi wa AICT Tanzania, baada ya kupata kura 622 kati ya 685 zilizopigwa. 
Aidha, katika mkutano huo, Mchungaji John Bunango alichaguliwa kuwa Askofu wa AICT Dayosisi ya Mwanza.  Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Askofu Daniel Nungwana kustaafu mwaka jana. Mchungaji Bunango alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Biblia Katunguru kinachomilikiwa na AICT.

No comments: