AJALI NYINGINE YA BASI, ABIRIA 48 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA

Wakati bado machungu ya ajali ya mabasi mawili yaliyogongana eneo la Sabasaba mkoani Mara wiki iliyopita yakiwa bado hayajaisha ambapo zaidi ya watu 39 walipoteza maisha, taarifa zimetufikia muda mfupi uliopita kwamba basi jingine limepinduka mkoani Tabora leo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 48.
Taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda, zinasema basi hilo mali ya kampuni ya Air Bus likitokea Dar es Salaam kwenda Tabora lilipinduka mida ya mchana wa leo baada ya kupoteza uelekeo kufuatia mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari chetu, inahofiwa basi hilo lilipinduka kufuatia kupasuka kwa gurudumu la mbele hali iliyosababisha kupoteza uelekeo na kutumbukia kwenye korongo ambapo abiria hao inasemekana walifariki eneo la tukio.
Taarifa zaidi za uhakika zitakujia hapa hivi punde.

No comments: