WAFUNGWA WADAIWA KUNYIMWA HAKI ZAO



Wafungwa wengi hawapewi haki zao za msingi miongoni mwake, ikiwa ni kukaa muda mrefu magerezani na mahabusu bila kuonana na ndugu zao.
Aidha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imetaja polisi kuwa chanzo cha uvunjaji wa sheria kwa kukamata wahalifu bila  kujitambulisha na pia  kutumia nguvu wanapochukua maelezo kwa mtuhumiwa.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mary Massay aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa unaojulikana kama ‘Luanda Guideline’ kupitisha muongozo wa sheria zilizoandaliwa nchini Angola.
Massay alisema Tume ilitembelea katika mahabusu na magereza ya nchini walitambua kuwa wafungwa wengi wamekaa gerezani bila ya kuonana na ndugu zao pamoja na kwamba wanahaki hiyo.
Kwa mujibu wa Massay, mkutano huo ulihusisha nchi tano za Afrika, huku wahusika kutoka jeshi la polisi na magereza hawakufika katika mkutano huo licha ya kwamba walitakiwa kuhudhuria.
Kamishna kutoka Tume ya Haki za Binadamu Afrika, Med Kaggwa alisema kumekuwa na tatizo kubwa katika ufuatiliaji wa  haki za wafungwa na mahabusu.
Ilielezwa asilimia 50 ya wafungwa waliopo katika magereza nchini,  kesi zao zimechukua  miaka mitatu hadi minne kuisha.

No comments: