MTOTO MLEMAVU ATEKETEA KWENYE MOTO


Mtoto Rebecca James ambaye ni mlemavu wa miguu na aliyekuwa haongei, ameteketea  hadi kufa baada ya nyumba yao kuwaka moto. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema moto huo ulizuka ghafla juzi huko Magomeni Kagera kwenye nyumba hiyo inayomilikiwa na Rashid Khalfani (64), mkazi wa Magomeni. 
Alisema moto huo uliteketeza chumba cha kulala cha binti huyo na ulimuunguza hadi kufa akiwa ndani ya chumba hicho.
Alisema kwa mujibu wa mama wa watoto hao, Bahati Karuti aliwaacha watoto hao peke yao na kwenda kwenye shughuli zake za kuuza mkaa.  
Wakati huo huo, mwendesha bodaboda, Malongo Salum (25), amekufa papo hapo baada ya pikipiki yake yenye namba za usajili T 630 CKM kugongana na lori namba T 516 BWN eneo la Migombani, Segerea.

No comments: