KAMPUNI YAINGIZA TEKNOLOJIA MPYA KUPIGA VITA UJANGILI



Kampuni ya Huawei Technologies (T) Limited imeingiza katika soko la nchini teknolojia mpya ijulikanayo kama ‘enhanced LTE’, (eLTE) itakayopiga jeki serikali katika vita dhidi ya ujangili nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano uliojumuisha watu waishio ughaibuni uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Meneja Uhusiano wa Huawei,  Moses Hella alisema kifaa hicho kitawezesha kuleta mrejesho wa haraka wa mawasiliano katika nyakati muhimu.
Alisema kifaa hicho chenye uwezo wa kutuma video kwa haraka, kinaweza kuleta ufanisi mkubwa katika kampeni zinazoendelea nchini dhidi ya ujangili.
"Tumeleta katika soko la Tanzania teknolojia mpya iitwayo 'enhanced LTE' ambayo ni teknolojia ya mawasiliano ya kipekee. Hii ni muhimu hususani kwa ajili ya mawasiliano muhimu, inayowezesha utumaji wa habari kupitia video, ambayo hutumika hasa katika usafirishaji wa bidhaa muhimu au watu.
"Kwa kufunga kamera zisizo na nyaya na kupeleka mfumo wa simu wa ufuatiliaji katika hifadhi mbali mbali za taifa, kwa kiasi kikubwa itasaidia serikali katika vita dhidi ya ujangili," alisema Hella.

No comments: