KAMPUNI YA SBC WAZINDUA SODA MPYA

Kampuni SBC  watengenezaji wa vinywaji  baridi, imezindua  soda mpya aina ya Mirinda  Green Apple.
Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Godlisten Mende wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema kampuni hiyo ambayo ni watengenezaji  soda za Mountain Dew, Mirinda Orange, Pepsi, Seven Up wameamua kutengeneza soda hiyo mpya, lengo likiwa  ni kuwapatia wateja ladha mpya na nzuri kwa kila mtumiaji na yenye ladha ya tunda la apple.
“Wateja wetu wategemee ladha nzuri ambayo ni bora na itakayomfurahisha kila mtumiaji na inafaa kwa matumizi ya rika zote,” alisema Mende.
Aliongeza kuwa soda hii itaanzwa kuuzwa katika Mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma na baadaye itasambazwa nchi nzima.

No comments: