ELIMU YA UMMA NI MUHIMU KATIKA KUPATA KATIBA MPYA - BUTIKU


Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku, ametaka elimu kuhusu mchakato wa Katiba itolewe kwa Watanzania walio wengi, ili siku ya kupiga kura wafanye hivyo kwa dhamira yao wenyewe.
Butiku alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua Filamu ya Rasimu ya Pili ya Katiba, iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambayo imeshirikisha wasanii na itagawiwa kwa wananchi katika mikoa 20 nchini. 
Alisisitiza umuhimu wa elimu ya Katiba kwa Watanzania walio wengi, ili suala hilo lieleweke kwa Watanzania hao na siku ya kupiga kura ya maoni, wapige kura kwa dhamira yao wenyewe na sio kulazimishwa na mtu mwingine yeyote.\
Aliwataka wananchi baada ya kupatikana kwa Katiba, kutokubali kuona Katiba waliyoiandika ikivunjwa na mtu yeyote, badala yake waikubali kwani Katiba ndio itakayowalinda.
Kuhusu Bunge la Katiba, Butiko alisema ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wapitie Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya na kuiboresha kwa kuwa  imetokana na maoni ya wananchi ambao ndio watakaoipigia kura.

No comments: