Mwenyekiti wa Kamati
Namba Moja, Ummy Mwalimu, amesema pamoja
na Kamati yake kupitisha sura zote kwa kupata theluthi mbili kila upande, suala
la akaunti ya pamoja kwa Tanzania Bara na Zanzibar, hawakufanya uamuzi na
lilikuwa na hekaheka kubwa.
Alisema
wajumbe wa kamati hiyo, walitaka suala hilo liwekwe kiporo hadi baada ya
kukamilika kwa semina ya wataalamu wa masuala ya fedha jana kuhusu mgawanyo huo
wa fedha.
“Tunataka
tujue kwa sasa hali ikoje, changamoto zake na wapi kwenye kero. Kwenye suala
hili wajumbe walibishana sana na waliweka pembeni itikadi za vyama vyao vya
siasa,” alisema.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba 11, Hamad Masauni Yusuf, alisema Kamati yake
imeshapiga kura kwenye sura zote na changamoto kubwa waliyokumbana nayo, ni
suala la fedha za pamoja.
“Leo
(jana) tunategemea kupata elimu kutoka kwa wataalamu wa fedha na tukiona kuna
mambo muhimu, itatubidi tuitishe kikao cha dharura kufanya marekebisho. Lengo
ni pamoja na masuala ya fedha. Pia Muungano uimarishwe na kusiwe na mambo ya
kuutatiza na pande zote mbili zifaidike,” alisema.
Mwenyekiti
Kamati Namba Nne, Christopher ole Sendeka, ambaye hakuwepo kwa muda mrefu
kuhudhuria kamati kutokana na kuuguliwa na watu wa familia yake, alisema
kutokuwepo kwake hakupaswi kuonekana kuwa anaunga mkono
Ukawa.
Alisema
kwenye kamati yake kulikuwa na mjadala mkali na watu walikuwa wakali lakini
mwishowe walielewana vizuri.
Alitaja
maeneo yaliyosababisha wajumbe kuwa wakali kuwa ni ardhi, uraia pacha, masuala
ya wakulima na wafugaji na muundo wa Bunge.
Mwenyekiti
wa Kamati Namba Tatu, Dk Francis Michael, alisema kwenye Kamati yake
walipingana sana na kuvutana na kufanikiwa kupata makubaliano mazuri na kila
sura kupata theluthi mbili kwenye sura zote.
Wakati
huo huo Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta, alisema bunge hilo lina mamlaka
makubwa kuliko tume hiyo.
Amesema
hata wajumbe wa bunge hilo wanaoendelea kupitia rasimu hiyo, siyo mazuzu, wana
akili zao, wasomi na wapo watu wengi wanaotambua kazi hiyo na kuipongeza.
Sitta
alivunja ukimya huo na kutoa ufafanuzi jana mbele ya waandishi wa habari kwenye
viwanja vya Bunge mjini hapa, na kuongeza kuwa wananchi wameona rasimu ya
Katiba mpya, ina upungufu.
“Mimi
naelewa kuna watu wanakasirishwa sana na kazi tunayoendelea kuifanya, ni haki
yao kukasirika lakini kinachofanywa ni wananchi ambao hatukuwaalika, wanakuja
kwa makundi kuelezea wanachoona kuwa ni upungufu ndani ya rasimu, sasa haya
watayapeleka wapi?
“Hii
hali ya kuonekana sisi Bunge na Tume tupo hadhi moja si kweli, Tume ina mamlaka
yake lakini Bunge lina mamlaka makubwa zaidi ya Tume… waliotunga sheria waliona
ipo kazi inayofanyika pamoja na kufanya marekebisho ndio maana
wanachotoa
wao ni rasimu sisi tutakachotoa inaitwa Katiba inayopendekezwa.”
Alisema
dhana kwamba lolote likifanywa kwenye rasimu ni usaliti kwa nchi au
inachakachuliwa, msingi wake ni ghadhabu za mtu na uamuzi tu wa kuwaona waliopo
Dodoma ni mazuzu.
“Hapa
kuna watu wasomi wazuri tu wenye akili zao. Kusema tunafanya kazi ya Tume ni
upotoshaji mwingine wa watu wasiotakia mema Bunge Maalumu la Katiba. Sijui kwa
nini rasimu inapewa hadhi kama msahafu, wakati imeandikwa na binadamu tu ina
upungufu mkubwa.
“Mtaona
kuanzia Septemba 2 mijadala ya hoja itakavyokuwa.
Wananchi
wao wameona Tume haikuwatendea haki maoni yao waliyoyatoa, na waliona mahali pa
kwenda kwenye chombo cha juu zaidi nacho ni Bunge Maalumu la Katiba, tuna
wajibu wa kuwapokea kwani tupo kwenye kazi ya kutunga Katiba”.
Alisema
kazi inayofanyika, ni kutoa Katiba rafiki kwa wananchi na kutoa mfano wa
wasanii, ambao waliona pamoja na kutoa maoni kwa maandishi, hayakuzingatiwa na
Tume lakini Bunge kwa vigezo vyake, limeona inastahili.
“Wamekuja
wakitaka kwenye rasimu kuwekwe kipengele cha mali isiyoshikika, yaani haki miliki
bunifu nasi tumeona inastahili, lakini Tume waliiacha nasi tumeongezea kwenye
sehemu rasimu iliyoweka mali tu,” alisema.
Miongoni
mwa vipengele vilivyoongezwa kwenye rasimu hiyo, ni masuala ya Serikali za
Mitaa, yaliyotokana na andiko la aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba, ambayo yalipangwa kuwepo kwenye Katiba ya Serikali
ya Tanganyika, ambayo ni ardhi, mazingira, rasilimali za Taifa na haki za
watumiaji wa bidhaa.
No comments:
Post a Comment