RAIS KIKWETE AWAPA IDD EL FITRI WAZEE WASIOJIWEZA

Rais Jakaya Kikwete ametoa msaada wa chakula kwa kambi ya wazee wasiojiweza ya Bukumbi, wilayani Misungwi mkoani hapa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr.
Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mwenyekiti wa wazee hao na Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Mwanza, Jalia Mtani.
Alisema mwaka huu kwa niaba ya Rais Kikwete amekabidhi mchele  kilo 240, mbuzi wanne, mafuta ya kupikia lita 40 pamoja na chumvi vyote vikiwa na thamani ya Sh 665,000.
Alisema kituo hicho kina wazee wasiojiweza 114 ambao wengine waliugua ugonjwa wa ukoma na kutunzwa kwenye kambi hiyo.
Akizungumzia mkakati walionao katika kuhakikisha wazee hao wanapata huduma muda wote, Mtani alisema ni pamoja na kuhamasisha watu binafsi, taasisi za umma na NGOs kujitokeza na kuwasaidia.
Naye Mwenyekiti wa wazee hao, Richard Bushasha alimshukuru Rais kwa msaada huo wa chakula na kwamba na wao watafurahia sherehe hiyo pamoja na wenzao.

No comments: