WAFUGAJI NYUKI GAIRO SASA KUNEEMEKA

Wafugaji wa mazao ya nyuki katika wilaya ya Gairo , wameanza kufaidika baada ya Wakala wa Huduma za Misitu Wilayani  Gairo, Mkoa wa Morogoro kuanzisha  shamba darasa la kisasa la ufugaji nyuki.
Mpango huo  ulianza  Machi mwaka huu , na  jumla ya mizinga 40 imetundikwa eneo la msitu wa mradi huo ambapo tayari mizinga 10 kati ya hiyo ina nyuki.
Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Gairo, Elizabeth Njau, alisema hayo juzi  eneo la  mradi huo katika  Kijiji cha Msingisi. kilichopo wilayani humo.
Alisema, mradi huo umegharimu sh: milioni 5.6 ambapo sh: milioni 4 zikitolewa na Serikali kuu , wakati sh: milioni 1.6 ni thamani ya eneo la ardhi inayomilikiwa na Halmashauri chini ya utunzaji wa msitu wa asili uliotundikwa mizinga hiyo.
Hata hivyo alisema, shamba darasa la ufugaji nyuki limeanzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wafugaji nyuki wilayani humo ili kuwawezesha kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya nyuki asali n anta.
Kwa mujibu wa Ofisa Nyuki wa wilaya hiyo, mafunzo yanatolewa yanahusu ufugaji wa nyuki, uvunaji na ufungishaji wa kisasa wa asali ili kuhifadhi misitu.
“ Hadi sasa wawakilishi 20 wawili kutoka kila kikundi kutoka vikundi 10 vilivyoundwa hapa Gairo wamepatiwa mafunzo kwa vitendo ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa” alisema na kuongeza.

No comments: