Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania
imeandaa gulio la wazi kwa ajili ya mauzo ya bidhaa mbalimbali, ikiwemo simu na
ipad kuwezesha umma kupata bidhaa hizo kwa gharama nafuu.
Gulio hilo maarufu kwa jina la Vodacom Expo
linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia Juni 28, litakuwa
katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni.
Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salum
Mwalim alisema wanatarajia kuuza bidhaa hizo kwa bei ya chini tofauti na ya
soko.
"Mwaka jana kwa mara ya kwanza
tulipoitisha gulio hili tulishuhudia idadi kubwa ya watu wakifurika kwa ajili
ya kupata bidhaa mbalimbali za simu za mkononi, hali hiyo ilitupatia ujumbe
kuwa wazo tulilolibuni limepokelewa vema na Watanzania,” alisema Mwalim.
Alisisitiza lengo la kampuni ni kuhakikisha
wananchi wanakuwa na uwezo wa kumiliki simu bora na ya kisasa kwa ajili ya
mawasiliano ya sauti na huduma za intaneti.
No comments:
Post a Comment