VETA, CHUO CHA UTALII KENYA KUTOA MAFUNZOMamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Veta) imeingia makubaliano ya ushirikiano na Chuo cha Utalii Kenya (KUC) wa kutoa mafunzo, ushauri na kufanya utafiti kwenye sekta ya utalii.
Akizungumza baada ya kutiliana saini, Mkurugenzi Mkuu wa Veta,  Zebadiah Moshi alisema kupitia taasisi yao ya hoteli na utalii  (VHTTI) iliyoko Arusha, wamekubaliana na KUC kuendesha mafunzo, utafiti na ushauri katika sekta hiyo hususani huduma kwa wageni. 
Alisema makubaliano hayo pia yamelenga katika mpango wa kubadilishana wanafunzi na walimu, kujengea uwezo walimu wa ufundi stadi ndani ya mfumo wa Veta. 
Mkuu wa VHTTI, Flora Hakika alisema uamuzi wa kuanzisha ushirikiano huo umekuja wakati ambapo taasisi hiyo ina mahitaji ya kuzalisha rasilimali watu bora na yenye ustadi mkubwa katika sekta ya utalii na huduma kwa wageni.

No comments: