SAMSUNG WAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI

Kampuni ya Samsung Tanzania kitengo cha electroniki imewakabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na home theater, kamera, televisheni na simu za mkononi washindi 10 wa shindano lililofanyika Februari na Machi mwaka huu.
Makabidhiano hayo ya zawadi yalifanyika jana jijini Dar es Salaam katika duka kuu la Samsung lilipo katika Jengo la Quality Centre.
Mwakilishi wa Samsung Ibrahim Kombo alizitaja zawadi zinazoshindaniwa kuwa ni televisheni moja aina ya LED ya ukubwa wa nchi 32, galax tab, kamera, home theatre, microwave tatu na simu moja aina ya galax grand.
Washindi hao ni Hajra Mohamed aliyejishindia televisheni, Ibrahim Nassor aliyeshinda Tab, Tom Joseph aliyeshinda home theatre na Banza Hassan aliyeshinda kamera.
Wengine ni Kinal Kapor aliyeshinda kamera, Henry Henry aliyeshinda home theatre, Salma Abood aliyeshinda microwave, Yahya Seleman aliyeshinda kamera, Abubakar Ally aliyeshinda microwave na Hatibu Mbwana aliyeshinda home theatre.

No comments: