PAPA FRANCIS ATIMUA ASKOFU KWA KUDHALILISHA WATOTO

Balozi wa zamani wa Vatican katika nchi ya Jamhuri ya Dominica, Monsinyori Jozef Wesolowski ametiwa hatiani na Mahakama ya Kanisa Katoliki kwenye tuhuma za kudhalilisha watoto.
Kutokana na kutiwa hatiani huko amepokwa upadre wake. Monsinyori Wesolowski amekuwa kiongozi wa juu kuteuliwa na Papa kutiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ya kupokwa upadri.
Taarifa ya Vatican ilisema Monsinyori Wesolowski alikutwa na hatia na Mahakama hiyo ya Usharika wa Mafundisho ya Imani katika siku za hivi karibuni: kwa adhabu hiyo ina maana hataweza kutekeleza majukumu yake kama Padre.
Wesolowski amepewa miezi miwili ya kukata rufaa.
Lakini pia anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Vatican. Kwa kuwa ni Mwanadiplomasia wa Kipapa yeye ni raia wa mji wa nchi hiyo.
Papa alimrejesha Vatican, Wesolowski ambaye ni mzaliwa wa Poland Agosti 21, 2013 na kumfuta kazi baada ya Askofu wa Santo Domingo, Kadinali Nicolas de Jesus Lopez kumueleza Papa Francis kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa Wesolowski aliwadhalilisha watoto wa kiume akiwa Jamhuri ya Dominica.
Mamlaka za Dominican hatimaye zilianza uchunguzi  lakini hazikumshtaki. Poland, pia ilianza uchunguzi dhidi ya Wesolowski.
Wesolowski ni Ofisa wa Juu Vatican kuchunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji watoto na kesi yake iliibua waswali iwapo Vatican, kwa kumuondoka katika mamlaka ya Dominica ilikuwa ni kumlinda na kuanzisha uchunguzi wake kabla ya mamlaka za taifa hilo la Caribbean.
 Hata hivyo Vatican haijawahi kusema iwapo Wesolowski alishawahi kujitetea kuhusiana na tuhuma hizo na hajawahi kutoa mawasiliano yoyote kwa mawakili wake.
Kesi hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa umakini kwani Wesolowski alipewa upadirisho wake na Uaskofu na  Papa St John Paul 11 ambaye pia ni Raia wa Poland.

No comments: