NKASI WAITAKA 'CHAPA' YA DAGAA WA KIGOMA

Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri  wa Wilaya  ya Nkasi mkoani Rukwa, Kilimuka Garigunga anataka dagaa ambao wamepewa jina la ‘dagaa wa Kigoma’ kubadilishwa na kuitwa wa Nkasi kwa kile alichodai wanavuliwa zaidi wilayani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni ofisini kwake, alisema dagaa hao wavuliwao Ziwa Tanganyika,  wanapatikana zaidi wilayani kwake kuliko mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wake, Ziwa Tanganyika  katika  Wilaya ya Nkasi  lina ukubwa  wa kilometa  za mraba 3,749  ukiwa na ukanda wenye urefu wa kilometa 130.
Takwimu za makadirio ya Sensa  ya Uvuvi  iliyofanyika 2010-11  zinaonesha kuwa  eneo la Ziwa Tanganyika  upande  wa Wilaya ya Nkasi  lina uwezo wa kuvuliwa  tani 4,911 za aina mbalimbali za   samaki  wakiwemo  dagaa wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 7.0  kwa  mwaka.

No comments: