Mshambuliaji wa Chile, Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Brazil na kufanya matokeo kusomeka 1-1 katika mechi ya Kombe la Dunia hatua ya 16 Bora iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mineirao, huko mjini Belo Horizonte. Brazil ilisonga mbele kwa mikwaju ya penalti 3-2 ambapo upande wa Chile, Sanchez alikuwa miongoni mwa waliokosa penalti.

No comments: