Mshambuliaji wa Brazil, Hulk akituliza mpira kabla ya kuifungia timu yake bao la pili dhidi ya Chile katika mechi ya Kombe la Dunia hatua ya 16 Bora iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mineirao, mjini Belo Horizonte. Hata hivyo bao hilo lilikataliwa na mwamuzi Howard Webb kwa madai mpira huo ulitua mkononi mwa Hulk kabla hajafunga na hivyo kupeleka mechi hiyo kwenye muda wa nyongeza na kisha penalti ambapo Brazil ilifanikiwa kusonga mbele kwa mikwaju 3-2.

No comments: