AKANA KUMNG'ATA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI

Mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige(42) anayetuhumiwa kumng'ata mfanyakazi wake wa ndani,  amepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Alisomewa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Yohana Yongolo.
Wakili wa Serikali Tumaini Msikwa alidai kati ya Januari na Juni mwaka huu, maeneo ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni, Maige alimng'ata Yusta Kashinde(20) sehemu  mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu.
Mshitakiwa alikana maelezo aliyosomewa na kwamba aliiomba mahakama kumpatia dhamana.
Wakili Msikwa aliiambia mahakama kuwa dhamana ya mshitakiwa imezuiliwa kama awali kwa kuwa bado  wananchi wana hasira hivyo kuhofia usalama wake.
Hakimu Yongolo alisema shauri hilo litaanza kusikilizwa  Julai 10 mwaka huu.

No comments: