KAHAMISHIWA WODI IMEANDIKWA MOCHWARIJamaa mmoja kutoka kijijini alitumwa kuja Dar kufuatilia hali ya baba yake aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili. Alipofika akapigiwa simu na wenzake wa kijijini na mambo yakawa hivi. JAMAA: Haloo nimefika salama na tayari nimeshamuona mgonjwa wetu. KIJIJINI: Enhe, hali yake vipi? JAMAA: Anaendelea vizuri kabisa, afya yake imeniridhisha mno. KIJIJINI: Amelazwa wodi gani? JAMAA: Wodi aliyokuwa mwanzo siikumbuki vizuri, nakumbuka hii aliyohamishiwa sasa. KIJIJINI: Wodi gani hiyo? JAMAA: Nakumbuka mlangoni ilikuwa imeandikwa Mochwari!! Duh, kasheshe…

No comments: