Serikali
imetakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaotoa matusi na
kuwakashifu waasisi wa Muungano wa Tanzania ili kukomesha vitendo
hivyo
visijirudie tena.
Mmoja
wa wakimbiza Mwenge Kitaifa, Wito Mlemelwa alizungumza hayo wakati akiwaaga
viongozi wa Mkoa Kigoma ili kuendelea na mbio za Mwenge
mkoani
Katavi.
Mlemelwa
alisema kuwa katika mchakato wa Katiba mpya unaoendelea kumekuwa na matusi na
maneno ya kashfa kwa waasisi wa Muungano lakini wale wote waliofanya hivyo
hawajachukuliwa hatua yoyote na kwamba wakati umefika sasa wa jambo hilo
kutovumiliwa na hatua zinazostahili zichukuliwe.
Mkimbiza
Mwenge huyo alisema kuwa kama mtaani watu wa chini wakitukanwa wanakamatwa na
kuchukuliwa hatua kwa kuwekwa rumande kwa nini hao wanaotukana na kutoa kashfa
hadharani wasichukuliwe hatua, ametaka sheria ambayo ni msumeno kufanya kazi
yake sawa sawa na kwa uwiano.
Awali
Mkuu wa Mkoa Kigoma Issa Machibya alisema kuwa Serikali haitakubali kikundi cha
watu wachache kuvuruga amani na utulivu miongoni mwa Watanzania
kwa
ajili ya maslahi yao wakati wa mchakato wa Katiba mpya.
No comments:
Post a Comment