WANACCM WASIKITIKIA VIJEMBE VYA BUNGENI


Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wamesema wanasikitishwa na tabia za viongozi wa CCM badala ya kujadili matatizo ya wananchi bungeni wanaanza kutupiana vijembe na wapinzani. 
Akisoma risala katika uzinduzi wa shina la Pamba Road, mwanachama wa CCM, Exavery Rugina alisema kwa kufanya malumbano badala ya kujadili matatizo ya wananchi inawafanya waonekane hawajui watanzania wanahitaji nini wakati mategemeo ya Watanzania ni wabunge wa CCM. 
Aidha, alisema ni vema kuachana na viongozi wasiojua wajibu wao kwa watanzania kwa sababu wanataka chama kiwatumikie wao na si wao kukitumikia chama. 
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa shina hilo, Katibu Mwenezi wa kata ya Kivukoni, Hasan Malocho akiwataka wanachama wa CCM kuepuka watu wanaoponda muungano.

No comments: