WAFANYAKAZI WALIOGOMA TAZARA WAREJEA KAZINI

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wamerejea kazini wakitii amri ya mahakama na  jana safari za treni ya Dar es Salaam zilifanyika.
Aidha treni inayofanya safari zake kwenda Zambia na mikoa mingine zinatarajiwa kuanza kesho.
Baadhi ya abiria waliokuwepo katika kituo cha makao makuu Dar es Salaam kwenda Mwakanga walimwambia mwandishi kuwa wamefurahishwa na kuanza kwa safari hizo.
Aidha watu waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kukuta tiketi za kwenda mkoani walisema wameambiwa safari zote zitaanza Kesho.
“Kikubwa tumefurahishwa na mgomo kuisha na safari kurejea kama kawaida, tulishindwa kusafiri ila sasa hata kama ni Ijumaa hatuna budi kusubiri,” alisema Juma Abdalah.
Naye Esta Danford alisema alihitaji kwenda kumuona mama yake ambae ni mgonjwa Zambia na alishindwa kutokana na mgomo huu.
“Mama yangu ni mgonjwa sana kutokana na mgomo nilishindwa ila nashukuru kuona safari zimerejea naamini sasa nitakwenda kumuona mama,” alisema Danford.
Wafanyakazi hao ambao juzi walitangaza kusitisha mgomo huo ambao ulianza Mei 12 mwaka huu, baada ya mahakama kuubatilisha.
Ambapo wafanyakazi hao walikuwa wakigoma kudai kulipwa mishahara yao ambayo walikuwa wakiidai serikali.
Mgomo wa wafanyakazi ambao  serikali imedai  kupata hasara ya Sh bilioni 2.65.

No comments: