VODACOM YAZINDUA HUDUMA YA 'UHURU WA KWELI'

Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania imezindua huduma ya intaneti isiyo na kikomo na isiyojali aina ya simu inayotumika, ikiwa ni moja ya malengo ya kuongeza matumizi ya intaneti na upatikanaji wa taarifa kwa Watanzania.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, huduma hiyo iliyopewa jina la ‘Uhuru wa Kweli’ inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki na mwezi.
"Hii ni njia pekee kwetu sisi kuweza kuziba pengo la kidigitali lililopo
nchini mwetu,’’ alisema Meza na kuongezea, ‘’Tunatambua kwamba wateja wetu wanatumia simu za aina mbali mbali na hii itasaidia kutumia facebook, whatsapp, twitter na huduma nyinginezo bila kujali aina ya simu.”
Uhuru wa Kweli ni huduma ambayo inawaruhusu wateja wa Vodacom kununua vifurushi vya intaneti vya siku kwa Sh 1,000 vya wiki kwa Sh 6,000 na vya mwezi kwa Sh 20,000 tu.

No comments: