VIJIJI VYAUZA MAGOGO YA SHILINGI MILIONI 203


Vijiji vitano wilayani Kilwa katika Mkoa wa Lindi vilivyo kwenye mpango maalumu wa kusafirisha na kuuza magogo nje ya nchi, vimejipatia zaidi ya Sh milioni 203 kati ya mwaka jana na mwaka huu kutokana na mauzo hayo .
Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano katika mradi wa kuhifadhi na kuendeleza misitu ya asili, Abigail Wills alisema vijiji vya Kisangi, Liwiti na Nanjilinji A vinapeleka magogo ya asili hasa Mpingo kwa watengenezaji wa vifaa vya muziki nchini Uingereza na nchi nyingine za Ulaya. 
"Novemba mwaka jana tuliongeza kijiji kingine kiitwacho Likawage chenye msitu wa asili wenye ukubwa wa hekta 17,921" alisema Wills.
Kijiji cha Kikole kilichoingia kwenye mpango huo mwaka 2009 kimejipatia Sh  milioni 10. Aidha kijiji kilichonufaika zaidi ni Nanjilinji A kilicho na eneo la hekta 61,505 baada ya mauzo kilipata Sh milioni 112.5. 

No comments: