Ukosefu
wa vifaa vya kisasa vya kupimia hali ya hewa katika nchi nyingi za Afrika
ikiwemo Tanzania, umesababisha nchi hizo kushindwa kukabiliana na changamoto za
ongezeko la mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agness Kijazi, alisema hayo wakati wa
ufunguzi wa warsha ya wadau wa kitaifa kuhusu mpango wa mashauriano kwa ajili
ya huduma za hali ya hewa barani Afrika.
Mpango
huo umefadhiliwa na Serikali ya Norway, kwa ajili ya kuanzishwa kwa
huduma ya hali ya hewa ya kusaidia nchi za Afrika, kukabiliana na mabadiliko ya
hali ya hewa na kuongeza hali ya kupambana na ukame na mafuriko ya mara kwa
mara.
Akizungumza
kwa Niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Dk Kijazi alisema kuna
umuhimu wa wananchi kutumia taarifa za TMA kwa ajili ya maisha yao ya
kila siku.
Alisema
hata wakulima wanatakiwa kufuatilia taarifa hizo kwa ukaribu zaidi, ili kujua
mazao wanayostahili kulima kutokana na hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment