UANACHAMA EAC SUDAN KUSINI, SOMALIA KUANGALIWA UPYA OKTOBA


Majadiliano juu ya ombi la Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yameahirishwa hadi Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa nchi EAC huo,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema mjini hapa kwamba kucheleweshwa huko kutatoa nafasi kwa Sudani Kusini kufanya maandalizi ya kitaifa na mashauriano.
“Hata hivyo EAC imeshafanya maandalizi ya utaratibu na mpango wa majadiliano na Jamhuri ya Sudan Kusini juu ya nchi hiyo kuingizwa katika jumuiya,’’ alisema Kenyatta katika kikao Maalumu cha 12 cha wakuu wa EAC.
Alisema mgogoro uliozuka Sudan Kusini mwaka jana, bado unaendelea katika baadhi ya maeneo nchini humo.
‘’Hayo yanatokea licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini na pande zinazohusika katika mgogoro huo mapema mwaka huu,’’ alisema Kenyatta.
Alitoa mwito kwa pande zinazopigana kuheshimu hadidu za rejea za makubaliano ya amani yaliyofikiwa. 
Wakati huohuo Baraza la Mawaziri la EAC juzi lilisema kwamba asilimia 57.9 ya maamuzi na maelekezo ya wakuu wa nchi wanachama yemetekelezwa mpaka sasa.

No comments: